Sheria na Masharti ya Ziada ya Ramani za Google au Google Earth

Mara ya Mwisho Kurekebishwa: Julai 2022

Ili utumie Ramani za Google au Google Earth, lazima ukubali (1) Sheria na Masharti ya Google na (2) Sheria na Masharti haya ya Ziada ya Ramani za Google/Google Earth (“Sheria na Masharti ya Ziada ya Ramani za Google/Google Earth”). Sheria na Masharti ya Ziada ya Ramani za Google/Google Earth yanajumuishwa kwa kurejelea Ilani za Kisheria kuhusu Ramani za Google/Google Earth na API za Ramani za Google/Google Earth.

Tafadhali soma kila moja ya hati hizi kwa makini. Kwa pamoja, hati hizi zinajulikana kama “Sheria na Masharti”. Zinabainisha yale unayoweza kutarajia kutoka kwetu unapotumia huduma zetu na yale tunayotarajia kutoka kwako.

Ikiwa unatumia vipengele vya wauzaji pekee katika Ramani za Google kudhibiti Wasifu wako wa Biashara, basi Sheria na Masharti ya Wasifu wa Biashara kwenye Google yaliyo https://support.google.com/business/answer/9292476 yatatumika.

Tunakuhimiza usome Sera yetu ya Faragha ili uelewe vyema zaidi jinsi unavyoweza kusasisha, kudhibiti, kuhamisha na kufuta maelezo yako,

ingawa si sehemu ya Sheria na Masharti haya.
  1. Leseni. Mradi unafuata Sheria na Masharti haya, Sheria na Masharti ya Google yanakupa leseni ya kutumia Ramani za Google au Google Earth, ikiwa ni pamoja na vipengele vinavyokuruhusu:

    1. uangalie na uweke vidokezo kwenye ramani;

    2. uunde faili za KML na uweke safu kwenye ramani; na

    3. uonyeshe hadharani maudhui yaliyo na maelezo sahihi mtandaoni, katika video na machapisho.

    Kwa maelezo zaidi kuhusu mambo mahususi ambayo unaruhusiwa kufanya kwenye Ramani za Google au Google Earth, tafadhali angalia ukurasa wa ruhusa za Kutumia Ramani za Google, Google Earth na Taswira ya Mtaa.

  2. Matendo Yanayokatazwa. Hali yako ya kutii Sehemu hii ya pili ni sharti la kupata leseni ya kutumia Ramani za Google au Google Earth. Unapotumia Ramani za Google au Google Earth, huruhusiwi (au hupaswi kuwaruhusu wanaokuwakilisha):

    1. kusambaza upya au kuuza sehemu yoyote ya Ramani za Google au Google Earth au kubuni bidhaa au huduma mpya inayotokana na Ramani za Google au Google Earth (isipokuwa utumie API za Ramani za Google au Google Earth kulingana na sheria na masharti) yake;

    2. kunakili maudhui (isipokuwa uwe umeruhusiwa vinginevyo kufanya hivyo na ukurasa wa ruhusa za Kutumia Ramani za Google, Google Earth na Taswira ya Mtaa au sheria husika ya kumiliki haki za uvumbuzi, ikiwa ni pamoja na sheria ya "matumizi ya haki");

    3. kupakua kwa wingi au kuanzisha mipasho mingi ya maudhui (au kumruhusu mtu mwingine yeyote afanye hivyo);

    4. kutumia Ramani za Google au Google Earth kuunda au kukuza seti nyingine yoyote ya data inayohusiana na ramani (ikiwa ni pamoja na seti ya data ya ramani au uelekezaji, hifadhidata ya orodha za biashara, orodha ya wanaopokea barua pepe au orodha ya utangazaji kwa kutumia simu) ya kutumiwa katika huduma mbadala au huduma inayofanana kwa karibu na Ramani za Google au Google Earth; au

    5. kutumia sehemu yoyote ya Ramani za Google au Google Earth pamoja na bidhaa au huduma za watu wengine kwa ajili ya au kuhusiana na uelekezaji au udhibiti wa gari linalojiendesha katika wakati halisi, isipokuwa kupitia kipengele mahususi kinachotolewa na Google kama vile Android Auto.

  3. Hali Halisi; Kujichukulia Dhamana. Unapotumia data ya ramani, maelezo ya hali ilivyo barabarani, maelekezo na maudhui mengine ya Ramani za Google au Google Earth, unaweza kutambua kuwa hali halisi inatofautiana na matokeo ya ramani na maudhui, kwa hivyo fanya uamuzi wako mwenyewe na utumie Ramani za Google au Google Earth kwa dhamana yako mwenyewe. Unawajibikia jinsi unavyotumia huduma hizi na matokeo ya matumizi hayo, wakati wowote.

  4. Maudhui Yako katika Ramani za Google au Google Earth. Maudhui unayopakia, kuwasilisha, kuhifadhi, kutuma au kupokea kupitia Ramani za Google au Google Earth yanasimamiwa na Sheria na Masharti ya Google, ikiwa ni pamoja na leseni katika kifungu cha “Ruhusa ya kutumia maudhui yako”. Iwapo wewe ni mkazi wa Ufaransa, Sheria na Masharti ya Ziada ya huduma ya Tafuta na Google yanatumika kwa maudhui kama hayo ambayo yanapatikana hadharani kwenye huduma ya Tafuta na Google. Hata hivyo, maudhui yanayosalia tu kwenye kifaa chako (kama vile faili ya KML iliyohifadhiwa kwenye kifaa chako) hayapakiwi wala kutumwa kwa Google. Kwa hivyo, hayako chini ya leseni hiyo.

  5. Watumiaji wa Serikali. Iwapo unatumia Ramani za Google au Google Earth kwa niaba ya shirika la serikali, sheria na masharti yafuatayo yanatumika:

    1. Sheria Inayoongoza.

      1. Kwa mashirika ya serikali za mji au jimbo nchini Marekani na Umoja wa Ulaya, sehemu ya Sheria na Masharti ya Google yanayohusiana na sheria inayoongoza na mahala pa kesi haitatumika.

      2. Kwa mashirika ya serikali ya Marekani, sehemu ya Sheria na Masharti ya Google kuhusu sheria inayoongoza na mahala pa kesi itabadilishwa na yafuatayo:

        “Sheria na Masharti haya yatasimamiwa, kufasiriwa na kutekelezwa kwa mujibu wa sheria za Marekani bila kurejelea mgongano wa sheria. Kwa kiasi kinachoruhusiwa na sheria ya nchi ya Marekani: (A) sheria za Jimbo la California (isipokuwa kanuni za migongano ya sheria za California) zitatumika pale ambapo sheria husika za serikali ya nchi hazipo; na (B) mzozo wowote unaotokana au unaohusiana na Sheria na Masharti haya ya Ramani za Google au Google Earth utashughulikiwa tu katika mahakama za serikali za Kaunti ya Santa Clara, California, na wahusika wote wakubali eneo la mamlaka katika mahakama hizo.”

    2. Haki Zinazodhibitiwa na Serikali ya Marekani. Ufikiaji au utumiaji wote wa Ramani za Google au Google Earth unaotekelezwa na serikali ya nchi ya Marekani au kwa niaba yake, unatakiwa kutii sehemu ya "Haki Zinazodhibitiwa na Serikali ya Marekani" katika Ilani za Kisheria kuhusu Ramani za Google au Google Earth.