Ukurasa wa Ilani za Kisheria wa Data ya Biashara Zilizoorodheshwa

Zifuatazo ni ilani mbalimbali za kisheria ambazo Google inawajibishwa kutoa na sheria na/au mkataba ("Ilani za Kisheria"). Ilani za Kisheria zimejumuishwa kwa kurejelewa katika Sheria na Masharti ya Google Kwa kutumia bidhaa au huduma ya Google inayojumuisha data ya biashara zilizoorodheshwa, ikiwa ni pamoja na, lakini sio tu, vipengele vya programu za vifaa vya mkononi kama vile Zana ya Google ya Kutambua Mpiga Simu ('Huduma"), unakubali kuzingatia Ilani hizi za Kisheria. Isipokuwa kama imebainishwa vinginevyo, masharti yanayotumika katika Ilani za Kisheria yana maana iliyofafanuliwa katika Sheria na Masharti ya Google.

  1. Data ya Biashara Zilizoorodheshwa.

    1. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji, Denmark, Israeli, Luxembourg, Monaco na Morocco.

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Ufaransa, Ujerumani, Uholanzi, Ubelgiji, Denmaki, Israeli, Lasembagi, Monaco na Moroko, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Kapitol S.A. (inayotambulika kibiashara kama Infobel) ("Maudhui ya Infobel"). Haki za uvumbuzi katika Maudhui ya Infobel zinamilikiwa na Kapitol S.A au watoa leseni wake. Maudhui ya Infobel yanaweza tu kutumika kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya Kapitol S.A. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na Kapitol S.A na una maswali yoyote kuihusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    2. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Brazil

      Unapotafuta orodha zilizoko nchini Brazil, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na orodha za biashara na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na TeleLista S/A. Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na TeleLista au watoa leseni wake na yanaweza tu kutumika kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yanayotumika ya TeleLista. Ikiwa unajua ya kwamba orodha yako ya biashara imetolewa na TeleLista, na una maswali yoyote kuihusu unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    3. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Uturuki

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Uturuki, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Turkey Yellow Pages (Yellow.com.tr). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Turkey Yellow Pages au watoa leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya Turkey Yellow Pages. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na Turkey Yellow Pages na una maswali yoyote kuyahusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    4. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Kenya

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Kenya, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Yellow Pages Kenya Ltd (www.yellow.co.ke). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Yellow Pages Kenya au watoa leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yanayotumika ya Yellow Pages Kenya Ltd. Ikiwa una maswali, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    5. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Misri

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Misri, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Egypt Yellow Pages Limited (yellow.com.eg). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Egypt Yellow Pages Limited au watoa leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya Egypt Yellow Pages Limited. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na Egypt Yellow Pages Limited na una maswali yoyote kuyahusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    6. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Saudia

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Saudia, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Al Wahda Express Saudi Arabia (www.daleeli.com). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Al Wahda Express Saudi Arabia au watoa leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya Al Wahda Express Saudi Arabia. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na Al Wahda Express Saudi Arabia na una maswali yoyote kuyahusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    7. Orodha za biashara kwenye Google nchini Bulgaria

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Bulgaria, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na New Europe Directories Bulgaria EOOD (www.goldenpages.bg). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na New Europe Directories Bulgaria EOOD au watoaji leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na mengine ya New Europe Directories Bulgaria EOOD yanayoweza kutumika. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na New Europe Directories Bulgaria EOOD na una maswali yoyote kuyahusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    8. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Italy

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Italy, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na SEAT Pagine Gialle SPA (www.paginegialle.it). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na SEAT Pagine Gialle SPA au watoaji leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya SEAT Pagine Gialle SPA. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na SEAT Pagine Gialle SPA na una maswali yoyote kuyahusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    9. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google katika Jamhuri ya Ireland

      napotafuta biashara zilizo katika Jamhuri ya Ireland, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Central Index (www.centralindex.com) na YourLocal.ie, majina ya biashara ya Touch Local Ltd. Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Touch Local Ltd. au watoaji leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na msharti yoyote husika ya Touch Local Ltd. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na Touch Local Ltd. na una maswali yoyote kuyahusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    10. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google katika Jamhuri ya Czech

      Unapotafuta biashara zilizo katika Jamhuri ya Cheki, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Zlaté Stránsky (ZlateStransky.cz). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Zlaté Stránsky au watoa leseni wake, na zinaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya Zlaté Stránsky. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na Zlaté Stránsky na una maswali yoyote kuihusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    11. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini India

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini India, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na INFOMEDIA Yellow Pages (www.yellowpages.co.in) na/au IndiaCom (www.indiacom.com). Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na INFOMEDIA Yellow Pages au IndiaCom (panapofaa) au watoa leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya INFOMEDIA Yellow Pages au IndiaCom (panapofaa). Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na INFOMEDIA Yellow Pages au IndiaCom (panapofaa) na una maswali yoyote kuihusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    12. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini New Zealand

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Nyuzilandi, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Finda. Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Finda au watoa leseni wake, na zinaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya Finda. Ikiwa unajua ya kwamba maelezo yako ya biashara yametolewa na Finda na una maswali yoyote kuihusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    13. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Slovenia

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Slovenia, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na Monolit informacijski sistemi d.o.o. Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na Monolit informacijski sistemi d.o.o. au watoa leseni wake, na zinaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya Monolit informacijski sistemi d.o.o. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na Monolit informacijski sistemi d.o.o. na una maswali yoyote kuihusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.

    14. Biashara Zilizoorodheshwa kwenye Google nchini Taiwan

      Unapotafuta biashara zilizoko nchini Taiwan, matokeo yako ya utafutaji yanaweza kujumuisha maudhui (ikiwa ni pamoja na biashara zilizoorodheshwa na maelezo yanayohusiana) ambayo yametolewa na HongKu Info Co. Ltd. - www.ipeen.com.tw. Haki za uvumbuzi katika maudhui haya zinamilikiwa na HongKu Info Co. Ltd. - www.ipeen.com.tw au watoa leseni wake, na yanaweza tu kutumiwa kulingana na Sheria na Masharti haya na sheria na masharti yoyote husika ya HongKu Info Co. Ltd. - www.ipeen.com.tw. Ikiwa unajua maelezo uliyo nayo ya biashara yametolewa na HongKu Info Co. Ltd. - www.ipeen.com.tw na una maswali yoyote kuyahusu, unafaa kuwasiliana nao moja kwa moja.